Ee Mungu Msaada Wa Zamani
Ee Mungu Msaada Wa Zamani
Na tumaini letu
Makimbilio taabuni
Makao ya milele.
Kwa mkono wangu ulilinda
Watakatifu wako
Pasipo hofu walikaa
Wakikutegemea.
Zamani sana ulimwengu
Haujaumbwa bado
Tokea mwanzo ndiwe Mungu
U Mungu wa milele.
Miaka elfu mbele zako
Ni kama siku moja
Ni kama kesha la usiku
Kunapopambazuka.
Upesi siku zinapita
Huenda zao wote
Huenda zao kama ndoto
Haikumbukwi mchana.
Ee Mungu msaada Wa Zamani
U tumaini letu
Utuhifadhi taabuni
Na leo na milele.