Wakosaji fikirini

 


Wakosaji fikirini
Mwisho wa njia zenu!
Hamwogopi kupotezwa
Vibaya kuzimuni?
Rudini kwake Mwikozi!


Ref
Ndiye mwenye huruma,
Hawatupi wamjiao,
Njooni tu kwake Yesu!


Hapo mlipoyafuata
Mambo ya dunia hii,
Hamkuweza kuvivunja
Vifungo vya Shetani.
Rudini kwake Mwokozi.


Mambo yote hugeuka,
Tukimjua Mwokozi;
Twaondolewa makosa,
Tuwe wake Nwana tu.
Rudini kwake Mwokozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *