Nakuapia Yesu
Nakuapia Yesu, kukutumikia
Wewe u mfunzi wangu na rafiki mwema.
Sitaogopa vita nikikufuata
Siipotezi njia, ukiniongoza.
Dunia i karibu, Bwana unilinde,
Na majaribu mengi, yako pande zote.
Adui siku zote, ni ndani na nje,
Ee Yesu univute, Karibu na wewe!
Nazisikia sauti, zenye tamaa mbaya,
Na mambo ya dunia, yanivuta sana.
Ee Bwana sema nami, Furaha iwe kuu,
Nitakusikiliza, Wewe mlinzi wangu.
Waagana na wote, wakufuatao,
Kwamba uliko wewe, nao watakuwa.
Nami ninaagana, kukutumikia,
Yesu nisaidie, kukuandamia.
Hatua zako Bwana, naziona wazi,
Nizikanyage vema, hapa duniani.
Nishike hata mwisho, Ee Yesu Mwokozi,
Nichukue nikifa, na kwako mbinguni.