Mwokozi wangu, umekosa nini?
Wahukumiwa kama mwuaji.
Umeshtakiwa makosa
Uliyotenda?
Wapigwa sana, miiba taji lako,
Umetemewa mate, watukanwa,
wanyweshwa nyongo,tena siki kali,
Wasulibishwa!
Sababu gani unateswa hivi?
Makosa yangu yanakuumiza;
Mateso haya yako yanipasa,
Mimi mkosaji.
Ajabu kubwa sana tendo lako:
Mchungaji unateswa kwa ajili
Ya kondoo, Bwana unawalipia
Watumwa wako.
Tulipokuwa mateka ya mwovu,
Nawe ukaja ukatukomboa.
Twalistahili kufa kwa milele,
Ukatufia.
Mwokozi wangu nifanyeje mimi,
Niitangaze pote sifa yako?
Nakufuata nikutumikie
Maisha yote.