Wakristo wenzetu furahini nyoto mkiimba
Wakristo wenzetu furahini nyoto mkiimba,
Kwa sauti na moyoni “tuna ujumbe mwema,
Amezaliwa Kristo vyote vyamwabudu Yeye,
Aliyezaliwa siku ya leo.”
Wakristo wenzetu furahini nyoto mkiimba,
Kwa sauti na moyoni mmepewa Ujumbe,
Wa kumfurahisha, Lango lafunguliwa juu,
Na huyu mzaliwa, siku ya leo.
Wakristo wenzetu furahini nyoto mkiimba,
Kwa sauti na moyoni Yeye akaondoa
Hofu ya kaburinni akaleta tumaini,
Mwana huyu Yesu, siku ya leo.