Waimba, Sikizeni
1. Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni;
Wimbo wa tamu sana, Wa pendo zake Bwana;
Duniani salama, Kwa wakosa rehema.”
Sisi sote na twimbe, Nao wale wajumbe;
Ref
Waimba, sikizeni, Malaika mbinguni.
2. Ndiye Bwana wa mbingu, Tangu milele Mungu,
Amezaliwa mwili, Mwana wa mwanamwali;
Ametoka enzini, Kuja ulimwenguni
Mwokozi atufie, Ili tusipotee,
3. Seyidi wa amani, Ametoka Mbinguni,
Jua la haki, ndite, Atumulikiaye;
Amejivua enzi, Alivyo na mapenzi,
Ataka kutuponya, Kutuzalisha upya,
4. Njoo upesi, Bwana Twakutamani sana
Kaa nasi, Mwokosi Vita hatuviwezi
Vunja kichwa cha nyoka Sura zako andika
Tufanane na Wewe Kwetu sifa upewe.