Wachunga Walipolinda
Wachunga walipolinda
Kucha nyama zao,
Malaika mtukufu
Alishuka kwao.
Wakacha sana wachunga,
Akawatuliza,
‘Nawaletea habari
Ya kuwapendeza.‘
‘Mji ule wa Daudi
Leo amezawa
Mwokozi ni Kristo Bwana,
Ilivyoandikwa.‘
‘Huyo mwana wa Mbinguni
Ataonekana,
Amelazwa kihorini
Malazi hapana.‘
Alipokwisha yanena
Malaika hao
Waliimba wimbo huu
Usio na mwisho:
‘Enzi ni yake Mungu juu,
Na nchi salama,
Kwa watu nao radhi kuu,
Sasa na daima’.