Unahitaji Uhuru Kwel
Unahitaji Uhuru Kweli? Mwamini Yesu, Mwamini Yesu,
Ana uwczo kukukomboa, Sasa umwamini Yesu.
Ref
Bwana Yesu ana uwezo, Uwezo kwa damu;
Bwana Yesu ana uwezo, Kukuokoa Kweli.
Unahitaji kutakasika? Mwamini Yesu, Mwamini Yesu,
Utasafishwa kwa Roho wake, Sasa umwamini Yesu.
Uwe mwenye moyo safi mno, Uko uwezo wa ajabu;
Alama itoke kwa uwezo, Damuni mwa Mwana Yesu.
Ufanye kazi kwa Mfalme Yesu, Uko uwezo wa ajabu;
Uishi daima kumsifu, Damuni mwa Mwana Yesu.