Twendeni askari
1. Twendeni askari, watu wa Mungu,
Yesu yuko mbele, tumwandame juu,
Ametangulia Bwana Vitani,
Twende mbele kwani ndiye amini.
Ref
Twendeni askari, watu wa Mungu,
Yesu yuko mbele, tumwandame juu
2. Jeshi la shetani, Likisikia
Jina la Mwokozi, Litakimbia
Kelele za shangwe, Zivume nchini;
Ndugu inueni zenu sauti.
3. Kweli kundi ndogo, watu wa Mungu,
Sisi Na Mababa tu moja fungu,
Hatutengwi nao, moja imani, Tumaini
moja, na moja dini.
4. Haya mbele watu Nasi njiani,
Inueni nyoyo, Nanyi sifuni;
Heshima na sifa ni ya Mfalme,
Juu hata chini, sana zivume.