Twamsifu Mungu
1. Twamsifu Mungu kwa Mwana wa pendo
Aliyetufia na kupaa juu.
Refrain:
Aleluya! Usifiwe; Aleluya! Amin.
Aleluya! Usifiwe; utubariki.
2. Twamsifu Mungu kwa Roho Mtukufu,
Ametufunula Mwokozi wetu.
3. Twamsifu Mwana, aliyetufia,
Aliyetwaa dhambi akazifuta.
4. Twamsifu Mungu wa neema yoge,
Ametukomboa akatuongoza.
5. Tuamshe tena, tujaze na pendo,
Na moyoni uwashe moto wa Roho.