Sijui Sababu Ya Neema

 


1. Sijui sababu ya neema
Niliyopewa na Mungu,
Sikulistahili pendo lake,
Wala wokovu wa Yesu;


Chorus
Namjua niliyemwamini,
Na kusadiki kwamba aweza
Kulinda kilichowekwa
Amana kwake Bwana.


2.Sijui jinsi nilivyopewa
Imani ya kumwamini,
Neno lake Yesu lilileta
Amani yake moyoni;


3.Sijui jinsi Roho wa Mungu
Awaonyeshavyo watu,
Wapate kuzitambua dhambi,
Na kumfuata Yesu.


4.Sijui kama mambo yajayo
Yatakuwa ya salama,
Lakini nitamwamini Yesu
Mpaka tutaonana.


5.Sijui siku gani ya Bwana
Hapa atakaporudi,
Nitamngojea na imani
Hata kumlaki hewani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *