Sababu Elfu Kumi
Chorus
Hebu sifu Bwana E moyo wangu
Sifu jina lake; Imba kabisa
E moyo Abudu jina lake.
V1
Liinukapo jua siku mpya
Nitaimba wimbo wako
Cho chote kijacho maishani mwangu
Hadi jioni nitakuimbia.
V2
Mwingi wa upendo, mpole wa hasira
Jina lako kuu, moyo mpole
Kwa wema wako nitaimba milele
Sababu elfu kumi moyoni.
V3
Na siku ya mwisho nguvu zikiisha
Wakati wangu wa kuja kwako
Moyo wangu bado ‘takuimbia
Sababu elfu kumi milele.