Nmeitaji Mwokozi
1. Nimehitaji Mwokozi
Awe nami daima;
Nataka mikono yake,
Kunizunguka sana.
Ref
Hofu rohoni sina,
Aniongoza tena;
Sitanung’unika tena,
Nimfuate daima.
2. Nimehitaji Mwokozi,
Sina imani nyingi;
Atanifufusha moyo,
Wengine hawawezi.
3. Nimehitaji Mwokozi,
Mwendoni mwa maisha;
Katika mateso mengi,
Tena katika vita.
4. Nimehitaji Mwokozi,
Kiongozi njiani;
Kwa jicho aniongoze,
Ni’fike mbinguni.