Njooni Tumuabudu
1. Njoni na furaha, Enyi wa Imani,
Njoni Bethlehemu upesi!
Amezaliwa mjumbe wa Mbinguni
Ref
Njoni tumuabudu, Njoni tumuabudu,
Njoni tumuabudu Mwokozi.
2. Jeshi la mbinguni, Imbeni kwa nguvu!
Mbingu zote na zijae sifa!
Sifuni Mungu aliye mbinguni;
3. Ewe Bwana Mwema, Twakubarikia,
Yesu, utukufu uwe wako;
Neno la Baba limekuwa mwili;