Ni Mtu Wa Simanzi
1. Ni “Mtu wa Simanzi”,
Mwana wa mwenye enzi
Mwenye mengi mapenzi!
Asifiwe Bwana Yesu!
2. Akawa matesoni,
“Mungu mwana yakini
Akatoka Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
3. Akapata dhihaka,
Mzoea – mashaka
Ndiye yetu sadaka:
Asifiwe Bwana Yesu!
4. Tu wenye dhambi sana;
Kwake dhambi hamna,
Na Mungu twapatana:
Asifiwe Bwana Yesu!
5. Alikufa mtini,
Akalia dhikini,
Sasa yuko Mbinguni:
Asifiwe Bwana Yesu!
6. Punde atarejea,
Yesu kutunyakua,
Ndipo tutamwimbia:
Asifiwe Bwana Yesu!