Nakusalimu Kichwa
1. Nakusalimu kichwa kilichojaa damu,
Kilichovikwa taji la miiba mikubwa.
Kilichopata enzi kwa Mungu mbinguni,
kitukanwacho sasa matusi makali.
2. Bwana nayashukuru masumbuko yako,
Sababu ya kuteswa na kufa kuchungu.
Wewe umenishika nami nitakushika,
Mwisho nitakujia uliyenifia.
3. Nivike kama ngao nitakapo kufa,
Nione uso wako katika uchungu.
Ndipo nikutazame nikutumainie,
Anaye kufa hivi hapa kwa amani.