Nadumu Kwa Ahadi

 


1. Nadumu kwa ahadi zake Mfalme,
Yesu asifiwe kwa siku zote,
Nitamwimbia sana, atukuzwe
Kudumu kwa ahadi zake.


Ref
Dumu, dumu
Nadumu kwa ahadi za Bwana wangu
Dumu, dumu
Nadumu kwa ahadi za Mungu


2. Nadumu kwa ahadi, sina shaka,
Aahadi zisizokosa kabisa;
Kwa neno lake Mungu nitashinda;
Kudumu kwa ahadi zake.


3. Nadumu kwa ahadi, nafahamu
Nina utakaso mkamilifu;
Kudumu kwa uhuru wake Yesu,
Kudumu kwa ahadi zake.


4. Nadumu kwa ahadi zake Kristo,
Kwa milele nimefungwa na pendo;
Nitashinda kwa upanga wa Roho,
Kudumu kwa ahadi zake.


5. Nadumu kwa ahadi, sitakosa,
Sauti ya Roho nitasikia
Katika Mwokozi nimepumzika,
Kudumu kwa ahadi zake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *