Mwokozi kama mchunga
Mwokozi kama mchunga
Utuongoze leo;
Ututume malishoni;
Fanya tayari boma.
Bwana Yesu, peke yako
Umetuvuta kwako.
Tu wako, uwe rafiki,
Uwe mlinzi wetu;
Kundi lako ulilinde,
Tusivutwe na dhambi;
Bwana Yesu tusikie,
Tukiomba, samehe.
Umetuahidi kwamba
Utakubali watu,
Utawahurumia na
Utawapa neema;
Bwana Yesu, tunapenda
Kuwa wako.