Mungu Wetu Ndiye Ngome
Mungu wetu ndiye ngome, silaha tena ngao.
Atukingiaye shida, zitushikazo sisi.
Adui wa kale, afanya hila,
Za kutushinda; ni mwenye nguvu kuu,
Hakuna amwezaye.
Nguvu zetu hazifai, tunashindwa upesi.
Lakini tunaye shujaa, aliye mwenye nguvu.
Jina lake nani? Ni Yesu Kristo;
Mungu mwenyewe; hapana mwingine,
Ni mshindaji wa wote.
Shetani akikusanya majeshi yake kote;
Hatuogopi kabisa, kwani tutawashinda.
Mfalme wa dunia, akunja uso;
Ana hasira, lakini ni bure,
Neno moja tu laweza.
Neno la mungu lashinda, halitafuti msaada.
Mungu yu pamoja nasi, na roho ya hekima.
Wakitunyang’anya watoto na wenzi;
Mwili nayo mali, haidhoru,si kitu;
Twamfuata Yesu mfalme.