Mjini Mwake Daudi
I. Mjini mwake Mfalme Daudi,
Palikuwa zizi nyonge,
Mama alimzaa mtoto
Na horini akamlaza;
Mariamu mama yule
Yesu Kristo Mwana wake.
2. Ni muumba vitu vyote
Alishuka huku kwetu,
Nalo zizi nyumba yake
Na malalo ni majani,
Akakaa na masikini;
Yesu Mkombozi wetu.
3. Na alipokuwa mtoto,
Alimtii mama yake,
Akampenda siku zote
Kwa upendo mwingi sana.
Watu wote wa Kikristo
Wamfuate kwa upole.
4. Maana ndiye mfano wetu,
Alikua kama sisi;
Akajua udhaifu,
Na huzuni na furaha;
Shida na furaha zetu
Yeye anazishiriki.
5. Nasi mwisho tutamwona
Maana ametukomboa,
Mtoto huyu tumpendaye
Ndiye Bwana wetu juu,
Naye ametangulia
Tupafike akaapo.
6. Tutamwona si zizini
Pale ng’ombe wafungwapo,
Tutamwona juu mbinguni
Kuumeni pale Mungu;
Watu wake wamzunguka,
Kama nyota wanang’aa.