Deni yangu ya dhambi
1.Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa.
Kwake msalabani Nilipewa uzima.
Ref
Deni ya dhambi, Msalabani,
Ilimalizikia, Ni huru kabisa.
2.Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu,
Uwezo wa ushindi Hupatikana kwangu.”
3.Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee
Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.
4.Sina wema moyoni, Nidai neema,
Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.