Bwana nasikia kwamba

 


1. Bwana nasikia kwamba
umebariki wengi,
nami nakuomba sasa:
Nibariki na mimi!


Chorus
Na mimi na mimi
Nibariki na mimi.


2. Nipitie Baba yangu,
kweli mimi mkosaji,
Baba uingie kwangu,
nirehemu na mimi!


3. Nipitie, nakuomba,
Bwana Yesu, Mwokozi,
wakosaji wawaita,
uniite na mimi!


4. Nipitie Roho mwema
kweli mimi sioni,
mwenye nguvu za kuponya,
nipe nguvu na mimi!


5. Nipitie Baba yangu,
nakuomba kwa bidii,
umebariki wengine,
nibariki na mimi!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *