1. Watu wa Yesu, sifuni Bwana,
M-tangazeni, ulimwenguni,
Sifa za Yesu, zienee pote,
Mataifa yote, yamsifu Yesu..
2. Humilki pote, mbingu na n-chi,
Ufalme wake, hauna mwisho,
Wote wa mbinguni m-tukuzeni,
Msifuni daima hata milele..
3. Neema yake ni nyingi sana,
Upendo wake ni wa ajabu,
M-linzi, M-chunga,Mwokozi wetu
Mfarifi, Mwombezi na Kiongozi..
4. Fadhili zake zaonekana,
Anavikidhi viumbe vyake,
Vyakula, vinywaji ni vingi kwake,
Mwangaza na mvua atugawia..
5. Sifuni Bwana kamwimbieni,
Anastahili fahari yoge,
Heshima na pendo m-peni Bwana,
Mwokozi Mwombezi na Mfalme Yesu.