Kama ulivyoagiza

 


1. Kama ulivyoagiza
kabla kuuawa,
hivi nitafanya, Bwana
nitakukumbuka.


2. Wewe kwa ajili yangu
ulitoa mwili
katika mkate wako huu,
nitaukumbuka.


3. Vivyo damu ya thamani
Wewe ulitoa.
Katika kikombe hiki,
Nitaikumbuka.


4. Nitazamapo Golgota,
kuona msalaba,
na kipaji cha kafara
nitakikumbuka.


5. Siwezi kusahau jinsi
ulivyoumia,
kweli nikiwapo mzima
nitakukumbuka.


6. Kwa hiyo nakungojea
Ee Bwana kwa kuwa
ujapo mara ya pili
utanikumbuka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *