Heri Niwe Na Yesu

 


Heri Niwe Na Yesu sio fedha, dhahabu
Heri Niwe wake sio kuwa tajiri
Heri Niwe na Yesu Sio nyumba na mashamba
Heri aniongoze kwa mkono wake.


Ref
Kuliko Kutawala milki kubwa
Au kunaswa, dhambini nipotee
Ni heri niwe na Yesu, Kuliko chochote
Kiletwacho na hii dunia.


Heri Niwe Na Yesu sio sifa za dunia
Heri Niwe mwaminifu kwa mwito wake mkuu
Heri Niwe Na Yesu sio kuwa maarufu
Heri Niwe wa kweli kwa jina lake safi.


Yu bora kuliko waridi ulionawiri
Yu tamu kuliko asali itokayo kwa sega
Ndiye yote roho yangu huonea njaa
Heri Niwe Na Yesu niongozwe naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *