Tangu siku hiyo aliponijia
Tangu siku hiyo aliponijia,
Akae moyoni mwangu.
Sina giza tena, ila mwanga pia,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Refrain
Amani moyoni mwangu,
Kwa Yesu, Mwokozi wangu.
Sina shaka kamwe
Kwa sababu yeye…
Yu nami moyoni mwangu.
Sina haja tena ya kutanga-tanga,
Ndiye Kiongozi changu.
Dhambi zangu zote zimeondolewa,
Na Yesu Mwanawe Mungu.
Matumaini yangu ni ya hakika,
Katika Mwokozi wangu.
Hofu zangu na hamu zimeondoka,
Kwa kuwa ninaye Yesu.
Siogopi tena nikiitwa kufa,
Yu nami daima Yesu.
Mlango wa mbingu ni Yesu Mwokozi,
’Tapita humo kwa damu.
Nitaketi na Yesu huko milele,
Nimsifu Mwokozi wangu.
Nina raha moyoni majira yote,
Kwa Yesu Mwanawe Mungu.